Thou who didst call Thy saints of old
1.
Bwana uliyewaita
Watakatifu wako,
Wawe mitume, wachunga,
Walishe kundi lako;
Wanyonge na wenye hofu
Wakawa mashujaa,
Na wapole wa kunena
Wasiwe kunyamaza.
2.
Hata leo wawataka
Watakatifu wako,
Nawe wauliza tena,
Ni nani aliyeko
Alakaye nitume
Afundishe vijana?
“Ni tayari, Bwana wangu,
Nitume mimi, Bwana.”
3.
Nitume na mimi, Bwana,
Kama ulivyotumwa,
Habari ya msamaha,
Na dhambi kutubiwa,
Niwahubiri wakosa,
Na waliopotea,
Wokovu u wake Bwana,
Aliyewafilia.
4.
Astahiliye hapana
Kutamka habari,
Lakini Wewe waweza
Kutufanya tayari;
Neno lako tulijue,
Tupe na roho yako,
Hayatakua ya bure
Haya maneno yako.