62.Bwana Wa Mabwana

Bwana wa mabwana,
Mwenye nguvu sana
Twakusihi:
Neno la milele
Na liende mbele,
Waongoke tele
Kwa Mwokozi.

Tunaowaona
Wanavyopatana,
Kulipinga,
Hawataliweza
Neno, kulitweza:
Huwaje! Kucheza:
Na upanga?

Heri wajitunze
Ili wapatane,
Na Mwokozi;
Watafute sana,
Wapate kuona,
Yesu kuwa Bwana,
Mkombozi.

Mungu awaita
Wasije kukuta
Pigo lake;
Hakuona vyema
Wakose uzima,
Awape rehema,
Waokoke.

Mwenye utukufu
Tunamshukuru
Yeye pweke!
Nasifiwe sana,
Baba, naye Mwana,
Na wa tatu tena
Roho yake.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top