There is a green hill far away
1.
Kilima kando ya mji
Alikufa Bwana,
Kuokoa wakosaji
Akateswa sana.
2.
Kabisa hayasemeki
Mateso dhaifu:
Alikufa Mwenye Haki
Tupate wokovu.
3.
Alimwaga damu yake
Ili tuwe wema,
Tufae kukaa kwake
Mbinguni daima.
4.
Hatuna mwenye imani
Aliye na haki,
Wa kutosha yetu deni,
Rafiki Yesu tu.
5.
Alijua peke yake
Kufungua Mbingu
Ufunguo damu yake
Kondoo wa Mungu.
6.
Aliyetupenda hivyo
Nasi tumpende,
Tukamtumai vivyo
Nasi tumpende.