1.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mbona unaumia? Unateseka sana
Kwa ajili ya kuomba,
Waomba na jasho jingi likageuka damu
Chorus
Kumbe! ni dhambi zangu zinazokuumiza.
Bwana wangu, Mungu wangu,
Mimi leo, naja kwako
Ili niziungame.
2.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mboona unumía na mizigo mizito?
Umejitwalia Wewe msalaba mabegani
Kwa ajili ya watu.
3.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Mboona unatukanwa, wawambwa kama mwizi,
Bila tusi ukalia, Baba wangu, wasamehe:
Chukua roho yangu.
4.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Muda ulipofika, nchi ikawa giza,
Mbinguni pakatulía, angani pakawa kimya,
Watu wakaogopa.
5.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Jinsi ulivyoumwa, ukamwomba Baba,
Leo umeshinda kifo, sasa wapaa Mbinguni.
Naimba, Haleluya.