When the storms of life are raging
1.
Tufani inapovuma
Sana moyoni mwangu,
Huona pa kujificha
Mkononi mwa Mungu.
Chorus
Hunificha, hunificha,
Adui hatanipata;
Hunificha, hunificha,
Mkononi mwake.
2.
Pengine kuna taabu
Yanisogeza kwake;
Najijua si hasira,
Ni ya mapenzi yake.
3.
Adui wakiniudhi
Nami nikisumbuka,
Mungu atavigeuza
Vyote viwe baraka.
4.
Niishipo duniani
Ni tufani daima;
Anilindapo rohoni
Nitakaa salama.