Lord, thy word abideth
1.
Neno lako Bwana,
Ni imara sana;
Lilo latwongoza,
Lilo latufunza.
2.
Adui wabaya
Wakikaribia,
Neno lake Bwana
Ni ulinzi sana.
3.
Siku za dhoruba
Soma ukiomba;
Neno lake Bwana
Msaada sana.
4.
Ukilamini,
Hwenda na amani;
Chorus
Una na furaha,
Neno ni silaha.
5.
Ni furaha kweli,
Na wingi wa mali,
Neno lake Bwana
Kwa wasiokana.
6.
Neno la rehema,
Tukali wazima;
Faraja ipo papo,
Tufarikanapo.
7.
Tulijue sana
Neno lako, Bwana.
Hapa tukupende,
Kisha kwako twende.