When my life work is ended
1.
Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka;
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua Mwokozi nifkapo ng’amboni;
Alakuwa wa kwanza kunilaki.
Chorus:
Nitajuwa, nitajuwa, nikimwona uso kwa uso;
Nitajuwa, nitajuwa, kwa alama za misumari.
2.
Furaha nitapata nikiona makao
Bwana aliyotuandalia;
Nitamsifu Mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyonipa pahali Mbinguni.
3.
Nao waliokufa katika Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifkapo kwake huko Mbinguni,
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
4.
Milangoni mwa mji Bwana atanipisha,
Pasipo machozi wala huzuni;
Nitauimba wimbo wa milele; lakini
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.