Onward, Christian soldiers
1.
Twendeni askari, watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele, tumwandame juu;
Amelangulia Bwana vitani,
Twende mbele kwani ndiye amini.
Kiitikio
Twendeni askari watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele, tumwandame juu.
2.
Jeshi la Shetani, likisikia
Jina la Mwokozi, litakimbia,
Kelele za hangwe zivume nchini;
Ndugu inueni zenu sauti.
3.
Kweli kundi dogo, watu wa Mungu,
Sisi na mababa tu moja fungu;
Hatutegwi nao, moja imani,
Tumaini moja, na moja dini.
4.
Haya mbele watu nasi njiani,
Inueni myoyo, nanyi sifuni;
Heshima na sifa ni ya Mfalme,
Juu hata chini, sana zivume.