In the sweet by-and-by
1.
Nyimbo na tuziimbe tena,
Za aliyotupenda mbele;
Kwa damu ya thamani sana!
Mbinguni hwonana milele.
Nyimbo na tuziimbe tena,
Za aliyotupenda mbele;
Kwa damu ya thamani sana!
Mbinguni hwonana milele.
Chorus:
Twonane milele,
Twonane bandarini kule;
Twonane milele,
Twonane bandarini kule.
Twonane milele,
Twonane bandarini kule;
Twonane milele,
Twonane bandarini kule.
2.
Hupozwa kila aoshwaye
Kwa damu ya Kondoo yule;
Ataishi afurahiye,
Vya Yesu Mbinguni milele.
3.
Hata sasa hufurahia,
Tamu yake mapenzi yale;
Je, kwake tukifikilia,
Kutofarakana milele?
4.
Twende mbele kwa jina lake,
Hata aje Mwokozi yule;
Atatukaribisha kwake,
Tutawale naye milele.
5.
Sauti zetu tuinue,
Kumsifu Mwokozi yule;
Ili watu wote wajue,
Wokovu u kwake milele.