94.Siku Ya Mbingu Kujawa Na Sifa

One day when heaven was filled with His praises

1.
Siku ya Mbingu kujawa na sifa,
Dhambi zilizidi duniani;
Yesu akaja azaliwe mtu,
Awe na watu ulimwenguni.

Chorus
Alinipenda, alinifia,
Ameondoa na dhambi zangu;
Alikufa nipewe haki,
Yuaja tena Mwokozi wangu.

2.
Na siku moja walikwenda naye,
Wakamkaza Msalabani;
Aliumia, alilaibishwa,
Ili atuokoe dhambini.

3.
Siku hiyo wakamlaza chini,
Kaburini alipumzika;
Matumaini yetu wenye dhambi,
Ni Mwokozi, kwake twaokoka.

4.
Kaburi likashindwa kumshika;
Jiwe likatoka mlangoni;
Alifufuka kwa kushinda kwake,
Naye yuko milele Mbinguni.

5.
Siku moja atatujia tena;
Utukufu wake tutaona;
Atawaleta na wapenzi wetu;
Mwokozi wangu, tutaonana.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top