Down at the Cross
1.
Msalabani pa Mwokozi,
Hapo niliomba upesi,
Akaniondoa Mpenzi,
Mwana wa Mungu.
Chorus
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Akaniondoa Mpenzi, Mwana wa Mungu.
2.
Chini ya Mti msumbufu,
Niliona utakatifu,
Alinikomboa kwa damu,
Mwana wa Mungu.
Chorus
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu.
3.
Aliniondolea dhambini,
Ikawa kunikaa ndani,
Aliponifia Mtini,
Mwana wa Mungu.
Chorus
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Aliponifia Mtini, Mwana wa Mungu.
4.
Damu ya Yesu ya thamani,
Huniondoa makosani,
Hunionyesha wokovuni,
Mwana wa Mungu.
Chorus
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Hunionyesha wokovuni, Mwana wa Mungu.
5.
Hicho kijito cha gharama,
Leo jivike kwa kuzama,
Kwake uone uzima,
Mwana wa Mungu.
Chorus
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu,
Kwake uone uzima, Mwana wa Mungu.