98.Huyo Ndiye! Anashuka

Lo, He comes with clouds descending

1.
Huyo ndiye! anashuka,
Aliyetufilia,
Wengi waliokoka,
Wakimfurahia.
Aleluya!
Yesu atarudia.

2.
Sote tutamtazama,
Amekaa Kitini;
Nao waliomchoma,
Kumkaza Mtini,
Na kilio,
Wamuone enzini.

3.
Alama za kifo chake
Hata sasa anazo,
Na waaminifu wake
Wapendezewa nazo
Alipata,
Kwetu alama hizo.

4.
Wokovu utakiwapo
Sasa wapatikana,
Na watakatifu hao
Mbinguni wakutana
Kumlaki,
Ndiyo siku ya Bwana.

5.
Wakusujidie wote
Mbele ya Kiti chako,
Zako, Bwana, nguvu zote
Itwae miliki yako,
Njoo Bwana.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top