Look, ye saints, the sight is glorious
1.
Tazameni huyo ndiye,
Mwenye kushinda vita;
Haya, tumsujudie;
Nyara anazileta;
Watu wote msifuni,
Sasa yumo Kitini.
2.
Msifuni malaika,
Mtukuzeni sana;
Wote waliokoka
Watamsifu Bwana;
Watu wote msifuni,
Sasa yumo Kitini.
3.
Walimfanya dhihaka
Zamani wenye shari;
Kwao waliokoka
Ni Bwana wa fahari;
Watu wote msifuni,
Sasa yumo Kitini.
4.
Nyimbo nzuri, sikizeni,
Ni nyimbo za sifa kuu;
Za Bwana Yesu Kitini,
Kutawazwa, Yeye tu;
Watu wote msifuni,
Sasa yumo Kitini.