88.Ndiyo Damu ya Baraka

Blessed be the fountain of blood

1.
Ndiyo damu ya baraka, ituoshayo wakosa,
Kwake Bwana twaokoka, nasi twamsifu sasa;
Nimestahili hukumu, siwezi kujitakasa;
Nioshe katika damu, takuwa safi kabisa.

Chorus
Safi kabisa; safi kabisa!
Nioshe katika damu;
Takuwa safi kabisa.

2.
Yesu alivikwa miiba, na kuangikwa Mtini,
Na maumivu si haba yaliyompata chini;
Nataka kijito hicho niende kuoga sasa;
Ndicho kinitakasacho, nami ni safi kabisa.

3.
Baba, kweli nimekosa, moyo wangu ni dhaifu;
Dhambi ni nyingi kabisa, nipate wapi wokovu?
Yesu kijitoni pako naja naamini sasa;
Nioshe kwa damu yako, takuwa safi kabisa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top