At the Cross
1.
Sioni haya kwa Bwana
Kwake nitang’ara!
Mti wake sitakana
Ni neno imara!
Chorus
Msalaba ndio asili ya mema,
Nikatua mzigo hapo;
Nina uzima, furaha daima,
Njioni kufurahini papo.
2.
Kama kiti chake vivyo
Ni yake ahadi;
Aliyowekewa navyo
Kamwe, havirudi.
3.
Bwana wangu, tena Mungu,
Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu
Wala kunikana.
4.
Atakiri langu jina
Mbele za Babaye,
Anipe pahali tena
Mbinguni nikae.