80.Wamwendea Yesu kwa kusafiwa

Have you been to Jesus for the cleansing power?

1.
Wamwendea Yesu kwa kusafiwa,
Na kuoshwa kwa damu ya Kondoo?
Je, neema yake umemwagikiwa?
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo?

Chorus
Kuoshwa, kwa damu
Itakasayo ya Kondoo;
Ziwe safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo?

2.
Namwandama daima Mkombozi,
Na kuoshwa kwa damu ya Kondoo?
Yako kwa Msulubiwa makazi,
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo?

3.
Atakapokuja Bwana-arusi
Uwe safi kwa damu ya Kondoo!
Yafae kwenda Mbinguni mavazi
Yafuliwe kwa damu ya Kondoo.

4.
Yatupwe yalipo na takataka,
Na uoshwe kwa damu ya Kondoo;
Huoni kijito chatiririka
Na uoshwe kwa damu ya Kondoo?

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top