Jesus my Saviour, to Bethlehem came
1.
Yesu zamani Bethilehemu
Aliyezaliwa kwa aibu,
Ndiye Mwokozi wa ulimwengu,
Akaja kwa mimi.
Chorus
Akaja kwa mimi; akaja kwa mimi;
Ndiye Mwokozi wa ulimwengu,
Akaja kwa mimi.
2.
Yesu akafa Msalabani,
Kuniponya akalipa deni;
Ni la ajabu ya jinsi gani
Kunifa mimi!
Chorus
Kunifa mimi! kunifa mimi!
Ni la ajabu ya jinsi gani
Kunifa mimi.
3.
Ni Yeye Huyo tangu asili;
Na nilipolanga tanga mbali,
Alikuja kwa upole, kweli
Kuniita mimi.
Chorus
Kuniita mimi;
Alikuja kwa upole, kweli
Kuniita mimi.
4.
Yesu Kristo atarudi tena,
Hilo lanifurahisha sana,
Yeye Bwana akionekana
Kunijia mimi.
Chorus
Kunijia mimi; kunitwaa mimi;
Yeye Bwana akionekana
Kunijia mimi.