Jesus is our Shepherd
1.
Yesu atuchunga,
Mchunga wetu,
Naye atufuta
Machozi yetu;
Mkononi mwake
Hatuna hofu,
Daima twapata
Kwake wokovu.
2.
Yesu atuchunga,
Tumemjua,
Na sauti yake
Twaitambua;
Naye akituonya
Ni kwa upole,
Tu kondoo zake
Hata milele.
3.
Yesu atuchunga,
Aliwafia
Kondoo wakubwa
Na wana pia;
Kwamba awajua,
Kondoo zake,
Hutiwa alama
Ya damu yake.
4.
Yesu atuchunga,
Mikono yake
Imewaambata
Kondoo zake;
Hapati wadhuru
Adui yule,
Yesu awalinda
Hata milele.