62.Bwana Wa Mabwana

The everlasting gospel

1.
Bwama wa mabwana,
Mwenye nguvu sana,
Twakusihi:
Neno la milele
Na liende mbele,
Waongoke tele
Kwa Mwokozi.

2.
Tunaowaona
Wanavyopatana
Kulipinga;
Hawatalweza
Neno, kulitweza;
Huwaje! kucheza
Na upanga?

3.
Heri wajitunze
Ili wapatane
Na Mwokozi;
Watafute sana,
Wapate kuona
Yesu kuwa Bwana,
Mkombozi.

4.
Mungu awaita
Wasije kukuta
Pigo lake;
Hakuona vyema
Wakose uzima
Awape rehema
Waokoke.

5.
Mwenye utukufu
Tunamshukuru
Yeye pweke!
Nasifiwe sana,
Baba, naye Mwana,
Na wa tatu tena,
Roho yake.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top