Oh for a heart to praise my God
1.
Nipe moyo wenye sifa,
Sio wa utumwa;
Moyo ulionyunyizwa
Damu ya thamani.
2.
Moyo msikini, moyo
Wa kunyenyekea,
Moyo utawaliwao
Na Mwokozi pia.
3.
Wenye kutubu, mnyonge,
Sadiki, amini;
Kamwe, kamwe asitengwe
Akaaye ndani.
4.
Mpya, mwema na mawazo
Mwingi wa mapenzi,
Nawe uwe kielelezo
Moyo wa Mwokozi.
5.
Ni uule moyo wako;
Moyo wa huruma,
Yesu, natamani kwako
Kukujua vyema.
6.
Na ya midomo matunda
Yako, nipe nami;
Amani isiyokoma
Iwe yangu mimi.
7.
Nitie yako tabia,
Inishukie juu;
Jina lako nipe pia,
Ndilo la upendo.
8.
Ni wa Baba utukufu;
Mwana atukuke;
Na Roho Mtakatifu,
Utatu pweke.