I was a wondering sheep
1.
Nilikuwa kondoo aliyepotea,
Sikupenda zizi kamwe, ila kutembea
Nilikuwa mwana asiyesikia,
Sikupenda baba yangu wala kutulia.
2.
Na mchunga mwema alinitafuta,
Baba kwa mapenzi ndiye aliyenivuta;
Karibu ya kufa, kwa kiu na kwa njaa,
Waliniona mnyonge, waliniokoa.
3.
Yesu ni mchunga, mwenziwe hapana,
Aliosha taka zangu, dhambi nyingi sana;
Kwa vidonda vyangu alitia dawa.
Ndiye aliyenipata, na kwake nalindwa.
4.
Nilikuwa kondoo aliyepotea
Sasa nampenda Baba, na mchunga pia;
Kwanza nilitanga na kukosa sana,
Hivi nyumbani mwa Baba sipotei tena.