1.
Hata ndimi elfu elfu,
Hazitoshi kweli
Bwana Yesu kumsifu,
Kwa zake fadhili.
2.
Yesu, jina liwezalo
Kufukuza hofu;
Lanifurahisha hilo,
Lanipa wokovu.
3.
Jina hilo ni uzima;
Ni afya amani;
Laleta habari njema;
Twalipiwa deni.
4.
Yesu huvunja mapingu
Ya dhambi moyoni;
Msamaha, tena nguvu,
Twapata rohoni.
5.
Kwa sauti yake vile
Wafu hufufuka
Wakafurahi milele,
Pasipo mashaka.
6.
Ewe Yesu wangu Bwana,
Uwezo nipewe,
Kuhubiri kote sana,
Wote wakujue.