My God, I am Thine
1.
Ni wako Mungu!
Ni furaha kwangu,
Ni raha kumjua Mwokozi wangu.
Chorus
Aleluya enzi ndako;
Aleluya, Amin.
Aleluya, enzi ndako;
Rejea Yesu.
2.
Mwana wa Mungu
Ndiye fungu langu,
Na moyo hufurahi kwa Yesu wangu.
3.
Raha ya kweli
Ina jina hili,
Na aliyeshika, ana Mbingu kweli.
4.
Nimeingia
Mapendano haya,
Nimepata uzima na Mbingu pia.
5.
Nilipo chini,
Ni mwako kazini,
Hata nije kwako uliko Mbinguni.