Oh, how He loves
1.
Mmoja apita wote
Atupenda;
Zaidi ya ndugu wote,
Atupenda;
Rafiki wa duniani
Wote hatuwaamini;
Yesu kwa kila zamani
Atupenda.
2.
Kumjua ni uzima
Atupenda;
Jinsi ajaavyo wema
Atupenda;
Yeye ametununua
Kwa damu aliyomwaga,
Dhambini kutuokoa,
Atupenda.
3.
Sasa tunaye rafiki,
Atupenda;
Hupenda kutubariki,
Atupenda,
Twapenda kumsikia,
Atwita kukaribia,
Nasi tutamwamania
Atupenda.
4.
Husamehe dhambi zetu,
Atupenda;
Hushinda adui zetu,
Atupenda;
Anatwonea huruma.
Hatupati ila mema,
Anatwongoza salama
Atupenda.