I’ve a message from the Lord, hallelujah
1.
Ni ujumbe wa Bwana, Aleluya!
Wa maisha ya daima.
Amenena mwenyewe, Aleluya!
Utaishi ukitazama.
Chorus
Tazama! ishi sasa!
Kumtazama Yesu,
Amenena mwenyewe, Aleluya!
Utaishi ukitazama.
2.
Ni ujumbe wa wema, Aleluya!
Nawe shika, rafiki yangu!
Ni habari ya raha, Aleluya!
Mwenye kuinena ni Mungu.
3.
Uzima wa daima, aleluya!
Kwake Yesu utauona,
Ukimtazama tu, aleluya!
Wokovu u pweke wa Bwana.