Thou my everlasting portion
1.
Bwana, U sehemu yangu,
Rafiki yangu, Wewe,
Katika safari yangu
Tatembea na Wewe;
Pamoja na Wewe,
Pamoja na Wewe,
Katika safari yangu
Tatembea na Wewe
2.
Mali hapa sikutaka
Ili niheshimiwe,
Na yanikute mashaka
Sawasawa na Wewe
Pamoja na Wewe,
Pamoja na Wewe.
Heri nikute mashaka
Sawasawa na Wewe.
3.
Niongoze safarini,
Mbele unichukue,
Mlangoni kwa Mbinguni
Niingie na Wewe.
Pamoja na Wewe,
Pamoja na Wewe.
Mlangoni kwa Mbinguni
Niingie na Wewe.