The King of love my Shepherd is
1.
Ni Mfalme wa mapenzi
Ndiye anichungaye,
Sipungukiwi, hawezi
Kunipoteza Yeye.
2.
Kando ya maji mazima
Yeye huniongoza
Katika malisho mema
Daima hunilaza.
3.
Mara nyingi hupotea
Kwa ukaidi wangu,
Naye huniandamia,
Hunirudisha kwangu.
4.
Uvumilivu mwa mauti,
Sichi hatari kamwe,
Wewe Bwana huniachi,
Mwokozi wangu Wewe.
5.
Waniandikia meza
Neema kwako tele,
Kwa Wewe, yote naweza,
Na msalaba mbele.
6.
Kamwe hautapungua
Uule wema wako;
Mwisho, atanichukua,
Juu, niimbe kwako.