109. Nitaimba ya Yesu

My song shall be of Jesus

1.
Nitaimba ya Yesu,
Kwa rehema zake,
Baraka nyingi sana
Nimepata kwake;
Nitaimba ya Yesu,
Sadaka ya Mungu;
Alimwaga damu
Ukombozi wangu.

2.
Nitaimba ya Yesu
Hapa siku zote,
Nitakapokumbuka
Vyema vyake vyote;
Nitaimba ya Yesu
Hata mashakani,
Yeye atanilinda
Mwake ubavuni.

3.
Nitaimba ya Yesu
Niwapo njiani;
Takaza mwendo, hata
Nifike Mbinguni.
Nikiisha ingia
Mlangoni mie,
Yesu nitamwimbia
Mbinguni milele.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top