Abide with me
1.
Kaa nami, ni usiku tena;
Usiniache gizani, Bwana;
Msaada wako haukomi;
Nili peke yangu, kaa nami.
2.
Siku zetu hazikawi kwisha.
Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho hakikomi,
Usiye na mwisho, kaa nami.
3.
Nina haja nawe kila saa;
Sina mwingine wa kunifaa;
Mimi nitaongozwa na nani
Ila Wewe Bwana, kaa nami.
4.
Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote, si taabu;
Kifo na kaburi haviumi;
Nitashinda kwako, kaa nami.
5.
Nilalapo nikuone wewe,
Gizani mote nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi
Siku zangu zote kaa nami.